+255 788 673 456

info@cocoorganization.org

MSAADA WA MATUNDU 20 YA VYOO, SHULE YA MSINGI NKUNDI

Katika kupigania Haki jumuishi ya Hedhi salama, community for change organization (COCO) kwa kuungana na The Rukwa Foundation imefanikisha kufika katika shule ya msingi Nkundi ambayo Inakabiliwa na uhaba wa vyoo, na vilivyopo vikiwa na matundu machache kwa ajili ya wanafunzi.

Community For Change Organization imeungana na viongozi wa serikali ya kijiji cha nkundi kata ya kipande wilaya ya sumbawanga kuchangia ujenzi wa matundu ishirini(20) ya vyoo ili kusaidia wanafunzi katika shule hiyo ya Nkundi.