+255 788 673 456
Hiki ni Kijiji Cha kifinga kata ya mtowisa wilaya ya sumbawanga vijijini, Mkoa wa Rukwa kwa historia hakijawahi kupata maji safi na salama tangu kiumbwe mwaka - 1974, yaani mpaka leo ni miaka 50.
Hapa unapoona ni chemchem ndogo ambayo watu zaidi ya 3000 wanaponea hapo,
Kijiji hiki magonjwa ya tumbo na kuhara damu ilishakuwa ni janga kubwa kwao.
Serikali na wadau mbalimbali, ndani na nje ya nchi tuwasaidie hawa wanakijiji wapate maji safi na salama.
Nakaribisha wadau kuweza kuona namna ya kuwasaidia hawa wananchi.
© 2023 - Community For Change Organization. All right reserved.